Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuapisha Kisari Matiku Makori
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais
Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni.
Akimuapisha
Mkuu huyo wa Wilaya RC Makonda ameeleza kuwa wananchi wa Ubungo
wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo
ni kusogeza huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe anatatua
changamoto zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti
anazoletewa ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji
hivyo inabidi hajiridhishe kwanza.
Katika
hatua nyingine RC Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya wote kutoruhusu
wananchi kubomolewa nyumba zao mpaka kuwepo hukumu halali ya mahakama
kwani wananchi wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao, hivyo wakuu
wa wilaya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki
inatendeka kwa kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka
husika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi
wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa
atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na
rasilimali zilizopo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimwapicha Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo,Kisari Matiku Makori kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli
kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.Picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori akila kiapo mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais
Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi katiba na ilani ya
chama cha mapinguzi (CCM) Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori
mara baada ya kumwapisha leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya wa mkoa wa Dar es Salaam,leo
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na
kamati ya ulinzi na usalama ya jiji la Dar es Salaam.
Sign up here with your email