MRATIBU WA TASAF KINONDONI ATUMBULIWA - Rhevan Media

MRATIBU WA TASAF KINONDONI ATUMBULIWA


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amemuagiza Mkurugenzi wa manispaa hiyo kumvua madaraka Mratibu wa Mfuko wa TASAF wa manispaa hiyo ndugu Onesmo Oyango kwa kosa la kuiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni mia moja.
Ally Hapi, DC Kinondoni

Mratibu huyo anadaiwa kuisababishia serikali hasara hiyo kwa kuziingiza kaya zaidi ya mia tano za manispaa hiyo ambazo hazina sifa ya kupewa ruzuku kwenye mpango wa malipo ya fedha za kusaidia wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha wanaoishi wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni Mheshimiwa Ally Hapi meeleza kuwa watu wanaotuhumiwa kuchukua fedha hizo ni pamoja na watumishi wa serikali, watumishi kutoka sekta binafsi pamoja na wafanyabiashara mbalimbali lakini pia hata baadhi ya kaya zilizopokea fedha hazijulikani makazi yake maalum huku kaya nyingine zikichukua fedha zaidi ya mara moja.
Hapi amevitaka vyombo vya dola kufanya ukaguzi upya ili vyombo hivyo viweze kubaini mapungufu na udanganifu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa pamoja na baadhi ya wasimamizi wa TASAF wa manispaa ya Kinondoni kupitia mpango huo wa kuziwezesha kaya maskini na vilevile ameiomba TASAF kumfanyia uchunguzi mhusika aliyekuwa anatoa fedha hizo kwa kaya ambazo hazikuwa na sifa.
Previous
Next Post »