120 WAKUMBWA NA KIPINDUPINDU DODOMA - Rhevan Media

120 WAKUMBWA NA KIPINDUPINDU DODOMA

Zaidi ya wagonjwa 120 wanaugua kipindupindu katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma baada ya kupokea wagonjwa wapya watatu wakitokea katika mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dkt. Said Mawji imeeleza kuwa wagonjwa hao watatu wamelazwa katika kituo cha afya cha Lumuna na kufanya idadi kuongezeka tangu ugonjwa huo ulipoingia mkoani humo Oktoba 26 mwaka huu.
Watu wawili wameripotiwa kufariki ambao wote wanatokea wilaya za jirani, huku akitaja wilaya ambazo zimeathriwa na ugonjwa zikiwa ni pamoja na Dodoma mjini, Mpwapwa na Kongwa na kuwa wameandaa mikakati katika ngazi zote ili kutokomeza ugonjwa huo katika mkoa huo.
Previous
Next Post »