KUNDI LA UPNZANI LAMTAKA KABILA KUJIUZULU - Rhevan Media

KUNDI LA UPNZANI LAMTAKA KABILA KUJIUZULU

Rais Kabila
Kundi la wanaharakati nchini DR Congo limeanzisha kampeni mpya ya kumshinikiza rais Joseph Kabila kung'atuka mamlakani kulingana na ripoti za BBC Afrique.
Muhula wa pili wa kabila na wa mwisho kwa ujumla unakamilika tarehe 19 Disemba na wapiga kura wanatarajiwa kushiriki katika shughuli hiyo mnamo tarehe 27 Novemba ili kumchagua mrithi wake,lakini makubaliano ya kisiasa yalioafikiwa mwezi uliopita na kundi moja la upinzani yaliahirisha uchaguzi huo hadi mwezi Aprili 2018.
Lakini ukipinga makubaliano hayo muungano wa vuguvugu la kidemokrasia ulizindua kampeni ya ''Bye-Bye Kabila'' ili kumshinikiza kung'atuka muhula wake unapokamilika mwezi Disemba.
Mavuguvugu yalio nyuma ya kampeni hiyo -Filimbi,Lucha na Jeunesse du Rassemblement yamesema kuwa yataandaa maandamano dhidi ya serikali.
Hatua hiyo huenda ikasababisha makabiliano makali na vikosi vya usalama.
Mnamo mwezi Septemba,msako dhidi ya wale wanaoipnga serikali ulisababisha vifo vya watu 50.
Marie-Joel Essengo,kiongozi wa vuguvugu la Lucha aliambia BBC Afrique:Tutafanya maandamano ili kuwahamasisha miongoni mwa vijana ,katika uma wote hadi tutakapopata mabadiliko tunayohitaji.
Hatuwezi kusubiri na kufikiria kwamba bw. Kabila atepewa dakika moja ya ziada kuwa rais baada ya tarehe 19 Disemba.
Previous
Next Post »