IHF YAWANOA NYOTA WA MPIRA WA MIKONO NCHINI UGANDA - Rhevan Media

IHF YAWANOA NYOTA WA MPIRA WA MIKONO NCHINI UGANDA

Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Mikono nchini Uganda, UHF, Shirah Agonzibwe Richardson, ameililia Serikali kupitia Baraza la Michezo la NCS, kuboresha miundombinu ya mchezo huo, nchini humo.
Mkufunzi wa IHF Francisco Aguilera akifatilia mafunzo ya mpira wa mikono ufukwe wa Entebe

Richardson, amesema hayo baada ya kumalizika mafunzo ya wachezaji 28 ya mchezo wa mpira wa mikono, kambi iliyokuwa ikifanyika kwa wiki moja kwenye fukwe za Entebbe.
Mafunzo hayo yalisimamiwa na mkufunzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Mikono Duniani, IHF, Francisco Aguilera, kutoka Hispania, na kuridhishwa na vipaji vya Uganda, lakini akitaka viendelezwe, ili kufikia lengo la kukuza mchezo wa mpira wa mikono nchini Uganda.
Previous
Next Post »