MAHAFALI ya Saba ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yanatarajiwa
kufanyika kesho yakiongozwa na Mkuu wa chuo hicho, Rais mstaafu wa Awamu
ya Tatu, Benjamin Mkapa.
Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idris Kikula, wahitimu 4,839 watahudhuria katika chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2007.
Kati ya wahitimu hao, 57 ni wa Cheti, 394 Stashahada, 4,046 Shahada za Kwanza, 242 ni Stastahada za Juu, 62 Shahada za Uzamili na 17 Shahada za Uzamivu.
Profesa Kikula alisema mahafali ya mwaka huu yatakwenda sambamba na shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi chuoni hapo.
Pia alisema hadi sasa chuo kina jumla ya wafanyakazi 1,372, kati yao 744 ni wanataaluma na 629 ni waendeshaji.

Sign up here with your email