WAWILI WAUAWA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI - Rhevan Media

WAWILI WAUAWA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Tokeo la picha la WAKULIMA UGOMVI NA WAFUGAJIWakazi wa Rufiji mkoani Pwani wamekumbwa na taharuki baada ya kutokea kwa mauaji ya watu wawili mkulima na mfugaji wilayani humo na maiti zao kukutwa zimetupwa porini.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Wilaya Rufiji mkoani Pwani Juma Njwayo amesema mauaji hayo yametokea kwa siku mbili zilizopita ambapo yanahusu mkulima na mfugaji na maiti moja imetambuliwa.
Marehemu anatoka katika eneo la Ngorongo kata ya Kilimani na wa pili ametajwa kuuawa na wananchi wenye hasira kali na kueleza kuwa kamati ya ulinzi bado inawatafuta waliohusika na kitendo hicho.
Amesema mpaka sasa ni watu wawili ndio waliopoteza maisha na imefahamika mkulima ameuawa kwa kukatwa mapanga na mishale na mfugaji ameuawa kwa kuchomwa moto na raia wasiojulikana.
Amewataka wanachi waache kujichukulia sheria mkononi
Previous
Next Post »