HIZI HAPA GHARAMA ZINAZOTUMIKA KWA SIKU KUMLINDA TRUMP JIJI LA NEW YORK. - Rhevan Media

HIZI HAPA GHARAMA ZINAZOTUMIKA KWA SIKU KUMLINDA TRUMP JIJI LA NEW YORK.

trump-tower
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump anagharimikiwa na jiji la New York kiasi cha shilingi milioni moja dola za kimarekani kwa siku kutokana na ulinzi wa Polisi, kwa mujibu maofisa kadhaa wa jiji hilo na vyanzo hivyo vinasema gharama hizo haziwezi kushuka kutoka hapo nyumbani kwake kwa sasa.
Shirika la habari la CCN, limeripoti kwamba “kila rais anapaswa kuwa na ulinzi wa kisheria pindi anapomaliza muhula wake wa utumishi,” lakini ulinzi kwa Trump ni gharama maradufu kwa kuwa anaishi kati kati ya mji maarufu,
Watoto wa Trump na wajukuu zake wote kwa pamoja wanapata ulinzi wa kitaifa na itifaki zote na mke wake Melania na mtoto wake mdogo Barron anapanga kubaki jiji New York mpaka mwisho wa muhula wake wa shule, gharama zitabaki kuwa juu zaidi.
trump-firstdraft02-facebookjumbo
Trump mwenyewe ameweka wazi kwamba anapendelea kuendelea kufanya kazi kutokea katika jiji la New York kama ikiwezekana ambapo itaulazimu mji huo kuweka katika hali ya ulinzi wa kisheria zaidi,”amesema Meya wa Jiji hilo la New York, Bill de Blasio katika mkutano na vyombo vya habari ijumaa iliyopita.
Cha msingi hapa ni ulinzi na usalama, “ ni ulinzi kwa ajili ya rais mteule, familia yake na wasaidizi wake wote,” amesema de Blasio, kwa mujibu wa CNN, “ Hatujawahi kuwa na rais wa Marekani anaishi maeneo haya ya New York, au kuwa na kiongozi wa nchini anakuwa maeneo kila wakati,”
trump-tower
Share:
Previous
Next Post »