Novemba
24, 2016 imetajwa tarehe ya kesi ya Bodi ya Wadhamini ya Chama cha
Wananchi (CUF) dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Fransic Mutungi,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Prof.
ibrahim Lipumba pamoja na watu 11 waliokuwa wanachama wa chama hicho
ambayo itasikilizwa Disemba 6, 2016.
Upande wa wadaiwa wamejibu maombi ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, pamoja na kuipinga kesi hiyo dhidi yao.
Wakili
upande wa wadai ambao ni Bodi ya Wadhamini CUF, Juma Nassoro amesema
Mwanasheria Mkuu, Msajili wa Vyama vya Siasa na Prof. Lipumba pamoja na
wenzake wameweka kila mmoja ameweka mapingamizi kwa kutumia hoja
mbalimbali ikiwemo kuwa, Mahakama hiyo haikutoa kibali cha kufunguliwa
kwa shauri hilo.
“Upande
wa wajibu maombi akiwemo msajili, mwanasheria na Lipumba walijibu
maombi Novemba 17 na sisi tumejibu. Lakini pia kila upande umeweka
mapingamizi kwa hoja kadhaa ikiwemo kuwa
Mahakama
Kuu Kanda ya DSM haijatoa kibali cha kufungua shauri hili na kwamba
sisi baada ya kusoma hoja zao tumeona ni hoja za kupikwa hivyo tumeweka
kipingamizi,” amesema.
Aidha,
Wakili Nassoro amesema Bodi ya Wadhamini imemuomba Jaji Amma-Isario
Munisi anayeendesha kesi hiyo kujiondoa kutokana na sababu mbalimbali
ambazo hakuzitaja kwamba barua ya maombi haijamfikia jaji huyo rasmi.
“Wadhamini
wameomba jaji kujiondoa ili asiendelee kuendesha kesi hiyo ingawa barua
ya maombi haikuingia kwenye faili. Sababu za wadhamini kumtaka jaji
kujiondoa zipo sitazisema sababu hiyo barua haijamfikia,” amesema.
Amesema
tarehe ya siku ya kusikilizwa kesi itakapofika kitakachojadiliwa ni
ombi la wadhamini la kumtaka jaji kujiondoa na mapingamizi yaliyowekwa
na pande zote mbili.
Nassoro amesema kuwa ” Nimefungua mashtaka kwa niaba ya chama
Kama
hakutakuwa na nguvu ya ndani, ushindi uko wazi sababu tunavithibitisho
na madai yetu ni ya msingi na wadaiwa wao wana vitu vya kupikwa. Kuhusu
jaji kukataliwa ni jambo la kawaida katika kesi kama hizi.”
Sign up here with your email