Kundi la
kigaidi la Al-Qaeda limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wao mkubwa Farouq
al-Qahtani huko kaskazini Mashariki mwa Afghanistan katika mapigano na
vikosi vya marekani mwezi mmoja uliopita.
Huko mjini Washington wamethibitisha kifo hicho kutokea November 15 yalikuwa ni makabiliano adhimu.
Lakini Al-Qaeda wamesema kuwa mkewe na watoto waliuwawa pia japo hawakujulikana kijeshi.
Vikosi vya
Marekani vimeiweka Al-Qahtani mzaliwa wa Saudi huko Quatar kama mtu
wanayemtafuta sana kwao akituhumiwa kuhusika na mipango ya mashambulizi
huko Marekani na Ulaya.
Sign up here with your email