Wanajeshi maalum wa
Uturuki wamewatia mbaroni wanajeshi wanaoshukiwa kufanya jaribio la
kumteka rais Recep Tayyip Erdogan wakati jaribio la mapinduzi
lililotibuka, lilipoanza wiki mbili zilizopita.
Ripoti zinaarifu
kwamba takriban makomando 11 walitiwa mbaroni nje ya mkahawa wa Marmaris
ambapo rais Erdogan alikuwa ameenda likizoni, japo alitoweka baada ya
kudokezewa kuhusu mpango huo kabla ya makomando hao kumvamia.Maafisa wanasema ndege zisizokuwa na rubani na helikopta zilitumiwa kuwasaka watoro hao, baada ya kuonekana na wanakijiji wakiwinda ngiri katika eneo hilo la misitu.
Sign up here with your email