Raia mmoja wa
Nigeria aliyetuhumiwa kuanzisha ulaghai mkubwa wa mitandao, ambapo zaidi
ya dola milioni sitini ziliibwa, amekamatwa katika mji wa Port Harcourt
Kusini mwa nchi hiyo.
Kukamatwa kwake kulifaulu baada ya
ushirikiano wa pamoja kutoka kwa Polisi wa kimataifa- Interpol na
mamlaka kukabiliana na ufisadi nchini Nigeria.Polisi wa kimataifa - Interpol, wanasema kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 40 anayefahamika kama 'Mike', anaaminika kuhusika na ulaghai wa zaidi ya dola milioni 60 na ana matapeli wengi wanaofanya kazi katika mataifa mbalimbali duniani.
Mtandao wake mkubwa uko nchini China, bara Ulaya na Marekani na mojawepo ya ulaghai huo ni wa ulipaji fedha ambapo kampuni mbalimbali za kibiashara hulipa pesa katika akaunti inayoaminika ni halali, lakini kumbe akaunti hizo zinadhibitiwa na magenge hayo ya wahalifu.
Sign up here with your email