Marekani imefanya
mashambulio ya angani katika ngome za wapiganaji wa Islamic State nchini
Libya kufuatia ombi la serikali ya taifa hilo inayoungwa mkono na Umoja
wa Mataifa,Pentagon imesema.
Mashambulio hayo yalilenga ngome za kundi hilo zilizopo katika bandari ya Sirte.Waziri mkuu wa Libya Fayez al Sarraj katika hotuba ya runinga,amesema kuwa mashambulio hayo yalisababisha 'hasara kubwa'.
Mashambulio hayo ni ya kwanza yaliofanywa na Marekani yakipangwa na serikali ya Libya.
Sign up here with your email