UCHAWI WA PENSELI NA KARATASI KWENYE MICHORO AMAZING’ - Rhevan Media

UCHAWI WA PENSELI NA KARATASI KWENYE MICHORO AMAZING’



Dunia ni zaidi ya uijuavyo; ni mfululizo wa makala ambazo zinakuonesha vitu chini ya jua vyenye utofauti na pengine hujawahi kuviona au kufikiria uwepo wake. Lakini kupitia unapata kuviona vitu hivi na vinakopatikana popote duniani.

Leo tunakuletea michoro ya ubunifu zaidi iliyochorwa kwa kutumia panseli  na karatasi pekee na ukiitazama unaweza ukahisi ni picha iliyopigwa kwa kutumia vifaa vya kielekroniki. Amini ninachokwambia, hapo imetumika penseli tu na kipande cha karatasi na watu wakatoa kazi za kushangaza sana.

DIEGO FAZIO (Sensazioni)

Jamaa anaitwa Diego Fazio amechora mchoro huu akitumia penseli tu na karatasi na ameupa jina la ‘sensazion’ au sensations kwa Kingereza. Diego alichora mchoro huu kwa masaa 200 na ukiutazama moja kwa moja huwezi kuamini kuwa ni mchoro badala yake utasema ni mtu amepigwa picha. Watu na vipaji vyao.

STEFAN MARCU (Cat)

Jamaa naye anajulikana kwa jina la Stefan Marcu ambaye alianza kuchora michoro tangu akiwa na umri wa miaka 5, jina la mchoro ni ‘cat’ au paka kama unavyoweza kujionea paka anaonekana ametazama juu. Sio rahisi pia kuamini kuwa ni penseli na karatasi pekee ndio vimetumika.

GIACOMO BURATTINI (Clint Eastwood)

Kipaji kingine hiki toka kwa Giacomo Burattini ambaye amemchora  mzee huyo kwa kutumia penseli na kipande cha karatasi pekee na kwa haraka haraka huwezi kukubali kama ni mchoro tu, tena wa penseli.

Jiunge nasi

Previous
Next Post »