Nikisema Imoooooo…. kila mtu kwa wale wapenda burudani tunakuwa tunasomana poa na wikiendi hii hapa Tamasha la Fiesta linadondoka mkoani Mwanza kuangusha burudani kwa wakazi wote waishio humo na maeneo ya karibu.Kama ingekuwa nazungumzia wakulima ama wafugaji basi msimu huu hapa ama kipindi hiki bila shaka kingekuwa ni kipindi cha mavuno lakini kwa wale wapenda burudani hii ni ‘time’ ya kula bata baada ya kuwa na likizo ndefu tangu kufanyika kwa fiesta ya mwisho mwaka 2014.
Kwa sasa wigo wa mapato ya wasanii yameongezeka kwa kiasi fulani kupitia shows na ringing tones, lakini inapokuja suala la Fiesta hapa ndipo utakapogundua idadi kubwa ya wasanii neema inakuwa imewashukia na utaona tofauti kubwa miongoni mwao.
Kipindi cha Fiesta ngoma kali huwa zinadondoshwa na wasanii ili waweze kupenya kwenye chujio na hatimaye kuchaguliwa kuperform kwenye lile jukwaa la Fiesta 2016 kama ambavyo hadi sasa zaidi ya wasanii 20 wamekwishatambulishwa; nini siri ya kukurukakara za wasanii hawa katika msimu wa Fiesta? Madee Ally amekubali kujibu.
Sign up here with your email