KIGWANGALA ARIDHISHWA NA UTAFITI TWAWEZA. - Rhevan Media

KIGWANGALA ARIDHISHWA NA UTAFITI TWAWEZA.



Utafiti wa Twaweza juu ya Sauti za Wananchi unaonesha maoni chanya kutoka kwa wananchi kuhusu Sekta ya Afya nchini kuwa asilimia 18 ya wananchi wanaoripoti kuona upungufu wa madaktari katika vituo vya afya miezi mitatu iliyopita, ukilinganisha na asilimia 43 walioliona tatizo hili mwaka 2015.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala amepongeza utafiti wa wadau juu ya Sekta ya Afya hapa nchini ambapo amesema tafiti hizo zinasaidia serikali katika kupanga mipango yake thabiti na kufahamu wapi panamapungufu ili kuchukua hatua zaidi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utafiti wa Twaweza “Sauti za Wananchi”, Dk. Kigwagala amesema Serikali ya Awamu ya Tano, imejipanga kusaidia wananchi kupitia sera za afya hivyo kila mwananchi atapata huduma bora za afya licha ya changamoto zilizopo kwenye wizara hiyo ambayo kwa sasa inaboresha mifumo yake mbalimbali ikiwemo suala la bima ya afya kwa kila mtanzania na huduma bora za afya kuanzia ngazi ya chini.

“Matokeo haya ya Twaweza yameonyesha matokeo mazuri hii ni pamoja na huduma nzuri ikiwemo lugha ya kiutendaji kwa sasa imekua ni ya kiungwana zaidi tofauti na kipindi cha nyuma.  Serikali ya awamu hii ya tano imekuwa ikifanya kazi kwa kasi sana kwa sasa hatukai maofisini zaidi muda wote ni kazi tu” alieleza Dk. Kigwangala.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Twaweza Nelline Njovu amesema Twaweza wamezindua matokeo ya utafiti huo ambao uliendeshwa kwa njia ya simu katika mfumo wa Afya ambapo waliangalia mambo mbalimbali ikiwemo maboresho ya huduma za afya kwa mwaka 2015-16 ambayo yanajumuisha Serikali ya Awamu ya Tano tokea kuingia madarakani.

Previous
Next Post »