KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) inatarajia kuingiza nchini ndege zake mpya mbili mwishoni mwa mwezi ujao ,Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ujio wa ndege hizo utaleta mapinduzi makubwa kihuduma na kiutendaji kwa kampuni hiyo, huku shukrani zaidi zikielekezwa kwa Rais John Magufuli kwa jitihada zake za kufufua rasmi ATCL.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema Dar es Salaam jana kuwa ujio wa ndege hizo utairejesha kampuni hiyo kwenye biashara ya ushindani dhidi ya kampuni nyingine za ndege hapa nchini.Ndege hizo zinazotengenezwa na kampuni ya Bombardier ya nchini Canada zinatarajiwa kuingia nchini wiki ya tatu na ya nne ya Septemba, mwaka huu, zikipishana kwa wiki moja.
“Baada ya ujio wa ndege hizi hatuoni tena sababu ya sisi kukwama, tutakuwa tumeingia rasmi kwenye biashara ya ushindani kwa kuwa changamoto kubwa ya uhaba wa ndege ambayo imekuwepo kwa miaka kadhaa sasa itakuwa imeanza kutatuliwa,’’ alibainisha Itule.
Sign up here with your email