Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. George Simbachawene amewataka viongozi mbalimbali wanaostaafu kujitunza vizuri ili endapo serikali itahitaji kuwatumia tena isisite na iendelee kuwatumia wakiwa na afya njema.
Amesema hayo katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) kwa wakuu wa wilaya wastaafu pamoja na viongozi wengine wa serikali akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Bw. Edward Hosea.Simbachawene ametumia hadhira hiyo kueleza nia na matamanio ya serikali kwa wastaafu hao ikiwemo ile ya kuendelea kuwatumia katika shughuli mbalimbali.
Aidha Mh. Simbachawene amewataka wakuu wa wilaya kuhakikisha kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii inawahudumia vyema wastaafu wote nchini ili wasiwe katika hali mbaya kiafya na serikali kushindwa kuwatumia tena pindi wanapohitajika katika shughuli nyingine na kutokana na afya zao kudhoofika.
Sign up here with your email