Baada
ya taarifa kwamba Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amejiuzulu uenyekiti
kuzagaa,Hatimaye sasa taarifa hizo ni za kweli,ambazo yeye mwenyewe amethibitisha hilo.
Alipoulizwa
kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia kusitiza uamuzi wake wa kutaka
kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka kumi, alisema basi imetosha.
“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.
“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari."
Kumekuwa
na taarifa kwamba Manji ameamua kuachana na wazo lake la kuwekeza Yanga
kwa miaka 10 baada ya kuona hata baadhi ya viongozi wa serikali
wakimuandama kwa madai wanatumiwa na baadhi ya mamilionea.
Taarifa
nyingine zimeelezwa kwamba, wako wanachama wa Yanga ambao wanaona
hawatafaidika na maslahi yao binafsi kama Manji atawekeza, hivyo
wamekuwa wakipambana kuhakikisha haingii mkataba na kupewa nafasi hiyo
kwa kuwa inaweza kuwavuruga.
Awali,
kumekuwa na taarifa Manji ameamua kujitoa kwa kuwa kuna juhudi za chini
pia zinazohusisha hadi watu wengine wenye mamlaka katika soka ambao
wana hofu na uwekezaji wake.
Sign up here with your email