POLISI WAMZUIA MBUNGE WA CUF KUFANYA MIKUTANO. - Rhevan Media

POLISI WAMZUIA MBUNGE WA CUF KUFANYA MIKUTANO.

Yatosha

Jeshi la Polisi wilayani hapa limemzuia Mbunge wa Tanga, Mussa Mbarouk kupitia CUF kufanya mikutano ya hadhara kwa muda usiojulikana  kutokana na kile ilichoeleza kwamba inaweza kuhatarisha amani.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo amesema hayo  alipokuwa akizungumza na Mwananchi.pic+mbunge“Mkuu wa jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga (OCD) amesitisha mikutano ya hadhara ya mbunge huyo kwa muda usiojulikana kwa sababu  ameonyesha kwamba mikutano yake haina malengo na nia njema,” alisema Paulo.

Alisema mbunge huyo alimakatwa juzi jumapili baada ya kufanya mkutano wa hadhara Agosti 13 mwaka huu katika mtaa wa Madina kata ya Msambweni ambako alitoa matamshi yenye kuchochea chuki baina ya wananchi na Rais pamoja na vyombo vya dola.

Previous
Next Post »