NI KWELI SIMBA NA YANGA HAZIWEZI KUFANYA VYEMA BILA YA MO DEWJI NA MANJI - Rhevan Media

NI KWELI SIMBA NA YANGA HAZIWEZI KUFANYA VYEMA BILA YA MO DEWJI NA MANJI


simba vs yangaBURHANI MOHAMED

Tumekuwa tukipiga kelele miaka  miaka mingi juu ya klabu hizi ambazo ni timu kongwe zenye mashabiki wengi zaidi Tanzania,kelele zetu nyingi ikiwa ni klabu hizi ziweze kufikia mahali na kujiendasha kisasa zaidi.

Kwa wingi wa mashabiki walionao ni kitega uchumi tosha cha kuzipeleka klabu hizi mbele na kupata heshima kubwa barani Afrika na hata nje ya mipaka ya bara hili, Mimi si mtaalamu sana wa uchumi lakini naamini chanzo kikuu cha kujenga uchumi ni kuwa na rasilimali watu, Simba na Yanga zinashindwa vipi kutumia raslimali watu ambao ni wapenzi na mashabiki kujinufaisha?

Mjadala mkubwa unaondelea kwasasa ni juu ya Mo Dewj kutaka kuwekeza bilioni 20 ili amilikishwe klabu ya Simba, wakati hilo likiendelea Manji nae kajitokeza anataka akodishiwe klabu ya Yanga kwa miaka 10, hapa napata wakati mgumu kufikiria, ikiwa wafanyabiashara wakubwa kama Yussuf Manji na Mohamed Dewj wanajitokeza kutaka kumiliki timu hizi, basi lazima kuna maslahi makubwa yanayopatikana kupitia timu hizi kongwe, Sasa swali linakuja je, kipi ni bora timu kuwanufaisha watu wachache au timu kujitengenezea chanzo kikuu cha mapato kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho?

Kwanini tusitafute mfumo sahihi ambao utandelea kuzifanya klabu hizi kuendelea kuwa mali ya wanachama huku zikijiingizia kipato maradufu,naamini kinacho zikwamisha klabu hizi ni kukosa viongozi makini wenye maono ya mbalimbali, wanaoweza kuziongoza klabu hizi zijiendeshe kisasa zaidi kuliko kuwategemea watu wachache wenye nguvu ya pesa kutaka kutumia klabu hizi kujinufaisha zaidi.

Simba na Yanga haziwahitaji Mo wala Manji katika kufikia malengo yake bali zinahitaji viongozi waadilifu na wenye mawazo chanya ili kusonga mbele na kufikia malengo waliyojiwekea tangu kuanzishwa kwao.


Previous
Next Post »