Hali hiyo ilitokana na walimu kuomba mkutano kwa ajili ya kuhoji uongozi wa chama hicho ambao unatuhumiwa kujiingiza katika ufisadi.Kwa mujibu wa walimu hao, wameeleza mkutano huo uliitishwa na Katibu wa CWT wa wilaya hiyo baada ya wajumbe wa mkutano mkuu zaidi ya nusu kuudai.
Mkutano huo ulikuwa na ajenda moja ya kujadili kusimamishwa kwa mweka hazina wa chama hicho bila ridhaa ya wanachama.
Kwa maelezo ya walimu wameleza kuwa, uongozi wa CWT Mkoa wamekuwa wakijichotea fedha za chama hicho kwa matumizi binafsi bila kuwashirikisha wanachama.
Kutokana na wanachama kudai mkutano huo uongozi kwa kutafuta njia ya kuzima agenga hiyo wakilazimika kukimbila polisi.
Hata hivyo, mkutano huo ulivunjwa muda mfupi baada ya Samson Mkotya, mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapo kwenda polisi akiwa na zuio la Mahakama ya Wilaya ya Dodoma lilitolewa juzi jioni.
Mkotya ambaye ni mtuhumiwa wa ufisadi wa fedha katika za chama aliuambia mtandao huu kwamba, mkutano huo ulizuiliwa na Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, kupisha kesi ya msingi inayohusihana na uhalali wa mkutano huo.
“Mamlaka ya uamuzi wa Mkutano Mkuu wa Wilaya yapo chini ya Kamati ya Utendaji ya Wilaya na si chombo kingine chochote wala mtu mwingine yeyote,”amesema.
Maswi Rafael, Katibu wa CWT Wilaya amesema, mkutano huo umeitishwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na uliridhiwa na Katibu Mkuu CWT Taifa.
“Hawawezi kusema hauhusiki Katibu Mkuu ndiye mtendaji mkuu wa chama hivyo hawezi kuwa mpumbavu akaangalia mahali panabomoka panaharibika, wanachama hawapati huduma akaendelea kuruhusu mawazo ya kamati ya utendaji ambao hawana busara,”amesema.
Kuhusu zuio la mkutano huo amesema, zuio hilo aliliona jana wakati mkutano huo ukiwa umeanza.
Augustino Chamasi, Mwenyekiti wa Mkoa wa CWT amesema, Nkyota amekwenda mahakamani kuzuia mkutano huo usifanyike jana kwasababu anajua angeendelea kuumbuka.
“Ili kumaliza tatizo hili mkoa tulishauri kuitishwa kwa mkutano mkuu kama walivyoomba awali ili huyo mweka hazina mliomweka rehani kama kumfungua mmfungue atoke ili Katibu afanye kazi,”amesema.
Gidion Kusika, Mweka Hazina wa CWT Wilaya ya Dodoma aliyesimamishwa amesema, mkutano huo ulilenga kutoa hukumu juu yake kuhusu fedha za CWT alizojikopesha.
Soma gazeti la MwanaHALISI kila Jumatatu kwenye simu yako kupitial.
Sign up here with your email