BREAKING NEWS:RAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR, ABOUD JUMBE AFARIKI DUNIA - Rhevan Media

BREAKING NEWS:RAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR, ABOUD JUMBE AFARIKI DUNIA

 ALIYEKUWA rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kati ya tarehe 7 Aprili 1972 hadi 30 Januari 1984, Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia mchana wa leo nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Saalam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kimethibitishwa na mmoja wa wanafamilia ya marehemu.

Marehemu Jumbe atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuiongoza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar akichukua nafasi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu Abeid Aman Karume aliyefariki mwaka 1972.

Enzi za uhai wake akiwa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar alishirikiana na rais wa wakati huo wa Tanzania na mwenyekiti wa chama cha TANU marehemu Julius Nyerere kuanzisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvunja vyama vya TANU na ASP na kuunda chama kimoja cha CCM.
Previous
Next Post »