Kigamboni ni moja ya wilaya tano zinazoliunda jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni wilaya mpya inachangamoto zake ambazo zinahitaji utatuzi ili kuleta matumaini mapya ya kujitegemea kama wilaya mpya kwa wakazi wa Kigamboni.
Kila sehemu ina mwenyeji na kunausemi usemao utu uzima dawa, hivyo kwa kuzingatia hayo Mkuu wa wilaya hiyo mpya ya Kigamboni Hashimu Shaibu Mgandilwa amekutana na wazee wa wilaya hiyo na kuzungumza changamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya hiyo, ambapo ameeleza kuwa anahitaji Kigamboni mpya yenye ulinzi na usalama ikiwa yeye ni kiongozi wa ulinzi na usalama kiwilaya atashirikiana kikamilifu kupinga vikali matukio ya uhalifu ambapo amewataka wazee hao kuwataja bila uoga wahalifu kwani wao ndiyo wenyeji wanawafahamu zaidi, huku akiahidi kujitahidi kupambana na magaidi na maharamia wanatumia Kigamboni kama kambi ya kujificha na kutumia kigezo cha dini ya Kiislamu.
Suala la pili ambalo amehaidi kupambana nalo ni Uvivu haramu ambapo ameeleza kuwa wilaya ya Kigamboni imebarikiwa kuwa na eneo kubwa linalozungukwa na bahari hivyo baadhi ya wakazi wamekuwa wakitumia mabomu kufanya uvuvi haramu na kuua kizazi cha samaki kwa kuwavua samaki wadogo wadogo ambao hawaruhusiwi kisheria, suala la tatu ni bishara ya Magendo na uwepo wa Viwanda bubu ambapo ameeleza kuwa ili Kigamboni mpya ipatikane na iwe na maendeleo lazima ikusanye kodi hivyo uwepo wa viwanda bubu na biashara za magendo unaikosesha mapato Halmashauri hiyo, hivyo amewaomba wazee kushirikiana nae kupambana na hilo, pia amesisitizia suala la usafi kwa wakazi wa Kigamboni kwani bado hairidhishi hivyo ni vyema kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake.
Huku suala la nne kwenye kuunda Kigamboni mpya Mkuu wa Wilaya hiyo amewata wakazi hao kupima maeneo yao kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi ili kuepuka wavamizi na kuhaidi kuwa ataunda baraza jipya la ardhi ambalo litazishughulika changamoto hizo kwa ukaribu, suala la tano mkuu wa wilaya hiyo ya Kigamboni amehaidi kuwatafutia fursa za maendeleo wakazi hao ikiwemo elimu ya ujasiriamali, vilevile amewataka wakazi hao kuachana na suala la la uchimbaji wa mchanga hususani kwa kata ya Mjimwema kwani suala hilo limepelekea uharibifu wa miundombinu na pia vimewahi kuripotiwa vifo vya watoto ambao wamekuwa wakitumbukia kwenye mashimo yanayochimbwa na wakazi hao kwa ajili ya mchanga.
Kwa upande wa wazee hao wamekubali kushirikiana na Mkuu wa wilaya huyo kwa kila jambo, ili Kigamboni mpya iweze kupatikana kwa maendeleo ya wakazi wote bila kujali itikadi za aina yeyote ikiwemo dini, rangi, kabila, jinsia, umri na tofauti za kisiasa.
Sign up here with your email