Katika hali ambayo haikutarajiwa mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho
Gambo ameanza kumhujumu mkuu wa mkoa Bwana Ntibenda. Hali hiyo imetokea
leo eneo la nane nane Arusha,leo ndio siku ya uzinduzi rasmi wa siku ya
nane nane ambako ilitegemewa watumishi wa halimashauri kuhudhuria
sherehe hizo ambazo mgeni Rasmi ni Mkuu wa mkoa
Katika banda la halimashauri ya jiji la Arusha hakukuwa na mtendaji hata mmoja baada ya kuitwa kwenye kikao kingine na mkuu w wilaya ya Arusha bwana Gambo katika ukumbi wa chuo cha ufundi Arusha. Haikuweza kufahamika mara moja sababu ya mkuu wa wilaya kumtoroka bosi wake na kuitisha kikao kisicho na tija wakati akijua kuwa sherehe za nane nane ni za muhimu zaidi.
Baadhi ya watumishi walioenda kwenye kikao cha DC wamekerwa na tabia ya DC kujisifu kuwa yeye ndie mteule sahihi wa Rais na kuwa siku si nyingi atapandishwa cheo kuwa RC hivyo watumishi wote wamsikilize yeye vinginevyo atawahamishia Tandahimba au Chato.
Kitendo cha leo ni mwendelezo wa mgogoro wa chini kwa chini unaondelea kati ya mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa unaosababishwa na tabia ya DC kumuhujumu waziwazi RC na wakati mwingine kuongea maneno ya kashfa dhidi ya RC

Sign up here with your email