Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo
wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi
ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao
za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria,
kanuni na taratibu za Nchi.
Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za
makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo
yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1)
na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya
sare za majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha
wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya
ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi
hayo bila kibali kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la
“ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi,
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.
Aidha Jeshi la
Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa
na majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini
na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.
Jeshi la Polisi
linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya
ulinzi na usalama kuzisalimisha mara
moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.
Imetolewa
na:
Advera John Bulimba – Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Sign up here with your email