Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabulla akizungumza na wadau wa benki ya ACB jijini Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa huduma ya mikopo na kuboresha makazi kati ya Black wood na Benki ya ACB.
Mkurugenzi wa Mipango kampuni ya Black Wood, Zouhra akizungumza na wa wadau wa benki ya ACB na kampuni ya Black Wood jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa kampuni ya Black Wood inakukopesha Viwanja vilivyopimwa na vya bei nafuu kwa watu wote wenye kipato cha chini anaweza kupata kiwanja kilichopimwa na chenye miundombinu yote.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya ACB, Israel Chasosa akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo jijini Dar es Salaam leo kati ya Benki ya ACB na Kampuni ya Black wood katika kununua viwanja vya kuanzia shilingi milioni tatu tu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabulla, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya ACB, Israel Chasosa na Mkurugenzi wa Mipango kampuni ya Black Wood, Zouhra wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya ACB na wafanyakazi wa kampuni ya Black Wood jijini Dar es Salaam mara baada ya uzinduzi wa huduma ya mikopo ya kuboresha Makazi.
Sign up here with your email