Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati wa ziara
yake mkoani Tabora alitoa maagizo kadhaa kwa watendaji likiwemo agizo la
kufunguliwa kwa stendi ya mabasi Igunga ambayo ilikamilika na kuacha
kutumiwa kwa miaka 10.
Kufuatia
agizo hilo tayari SUMATRA kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi
cha usalama barabarani wameanza kuelekeza magari yote ya abiria
yanayopita Tabora eneo la stendi hiyo kuhakikisha yanapita jambo ambalo
limeanza kufanyiwa kazi kwa vitendo.
Akizungumza
wakati wa kukagua utekelezaji wa agizo hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri amesema SUMATRA washirikiane na jeshi la polisi
kuhakikisha kila gari la abiria linapita na dereva atakayekaidi agizo
hilo anyang'anywe leseni.
"Ni lazima mabasi yapite hapa stendi na yeyote atakayekaidi SUMATRA chukueni hatua na jeshi la polisi toeni ushirikiano kuhakikisha suala hili linafanikiwa'' Amesema Mwanri.
Aidha
kwa upande wao wananchi wamesema watanufaika sana kufuatia stendi hiyo
kuanza kufanya kazi kwa kuwa watafanya biashara mbalimbali kuzunguka
stendi hiyo.
Sign up here with your email