Orodha ya wachezaji ambao walikuwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc msimu uliopita na mikataba yao kufikia tamati baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara mei 22 tayari imetolewa ikiwataja nyota saba kutokuwepo tena kikosini msimu ujao.
Muda
mfupi uliopita, Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe amesema kuwa,
wachezaji saba wanaotajwa kwenye orodha hii ni wazi mikataba yao
imemalizika na klabu haitafanya tena mazungumzo yoyote na tayari
wamesha taarifiwa juu ya hilo.
“Mikataba
yao imemalizika, tumekwisha wataarifu kuwa hatutakuwa na mazungumzo
mapya, hili soka kutoka timu moja kwenda nyingine ni jambo la kawaida
hivyo tunawatakia kila la heri kwenye maisha mapya ya soka watakayo
kutana nayo” alisema.
Kwenye orodha hiyo yupo mlinda mlango Haningtony Kalyesubula, walinzi ni Yusuph Abdalah Sisalo,Deo Julius,Hamad Kibopile,Yohana Morris, Richard Peter Chundu na mshambualiaji Temmi Felix.
Katika
hatua nyingine Kimbe amesema kuwa klabu bado inafanya mazungumzo na
baadhi ya nyota ambao mikataba yao imemalizika lakini bado wanayo
nafasi ya kuendelea kukitumikia kikosi cha City kwa mujibu wa
mapendekezo ya kocha Kinnah Phiri, huku pia mazungumzo ya wachezaji
wengine ambao bado wana mikataba lakini hawapati nafasi ya kucheza
yakiendelea ili kuona ni jinsi gani wanaweza kupata nafasi ya kuendeleza
vipaji vyao.
Orodha ya wachezaji hao pamoja na wale wanaoendelea kuitumikia klabu itatolewa hapo baadaeSign up here with your email