KAMPUNI
ya Yono Auction Mart ya jijini Dar-es-salaam,imewatoa nje kwa nguvu
wanunuzi na wapangaji wa nyumba za serikali mkoani Singida, kwa kile
kilichodaiwa kuwa hawajamaliza kulipa madeni yao kwa wakati.
Wadaiwa
sugu watatu waliokuwa na mikataba ya kununua nyumba
TBA/SGD/GOVT/BDG/LC/VETA namba moja,mbili na tatu zilizoko katika maeneo
ya VETA mjini humo, wanadaiwa zaidi ya shilingi 20.9 milioni.
Mpangaji
mmoja ambaye amepanga nyumba namba TBA/SGD/BDG/SAB/9 iliyopo maeneo ya
saba saba mjini humo, anadaiwa shilingi 179,000.00.
Meneja
wa kampuni ya Yono tawi la Dodoma, Tatu Rashidi,alisema zoezi hilo la
kuwaondoa kwa nguvu wadaiwa sugu wa nyumba za serikali,linaendelea
kufanywa na kampuni ya Yona nchi nzima.Kazi hiyo wamekabidhiwa na Wakala
wa majengo Tanzania (TBA).
Meneja
wa kampuni ya Yono Auction Mart tawi la Dodoma,Tatu Rashidi,akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya zoezi la kuwatoa kwa
nguvu wadaiwa sugu wa nyumba za wakala wa majengo Tanzania (TBA) mkoani
Singida. Jumla ya watu watatu wenye mikataba ya kununua nyumba
hizo,wametolewa kwa nguvu kwenye nyumba zao zilizopo maeneo ya VETA,kwa
kushindwa kulipa madeni yao yanayofikia zaidi ya shilingi milioni 20.
“Kazi
hii ambayo ni endelevu,tumeianzia katika mkoa wa Dodoma na sasa tupo
mkoa wa Singida, tukimaliza, tunahamia mkoa wa Manyara. Lengo letu ni
kwamba watu walioingia mkataba wa kununua nyumba za serikali, wanamaliza
kulipa madeni yao.Hali kadhalika na wale waliopanga nyumba za serikali,
wamalize kulipa madeni ya pango”,alifafanua Tatu.
Alisema
wadaiwa sugu hao wanaotolewa kwa nguvu kwenye nyumba za serikali,
wakilipa madeni yao ndani ya siku 14,watakabidhiwa nyumba zao.
“Watakoshindwa
kulipa ndani ya muda huo,kampuni ya Yono itabidi kuuza kwa njia ya
mnada vyombo/mali zao ambazo tunavishikilia kwa sasa”,alisema.
Fundi
seremala akivunja mlango wa nyumba no.TBA/SGD/BDG/SAB/9 iliyopo maeneo
ya saba saba ambayo mpangaji wake anadaiwa shilingi 197,000.00.
Kwa
upande wake Afisa wa wakala wa majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Singida,
Mohammed Mloka,alisema wateja walioingia mkataba wa kununua nyumba za
serikali,wanapaswa kuheshimu masharti ya mikataba yao,ili kuondokana na
aibu na usumbufu wa kutolewa kwa nguvu kwenye nyumba hizo.
Mloka
alitumia fursa hiyo kuwataka wapangaji na walionunua nyumba za
serikali,kujenga utamaduni wa kulipa kodi na madeni ya ununuzi wa nyumba
hizo kabla ya kufikiwa na mkono wa Yono.
Imedaiwa
kwamba kampuni ya Yono, imepewa orodha ya nyumba zaidi ya 3,000 nchi
nzima za walionunua na wengine waliopangisha nyumba za wakala wa
majengo,ambao muda wa kulipa madeni,uliishapita.
Meneja
Uendeshaji wa kampuni ya Yono Auction Mart ya jijini Dar-es-salaam,
Atukuzwe Mhugo,akishiriki zoezi la kuwatoa nje kwa nguvu wadaiwa sugu wa
nyumba za wakala wa majengo Tanzania (TBA) za mjini Singida.
Vijana
wakishiriki kutoa vyombo kwenye nyumba ya wakala wa majengo Tanzania
(TBA) TBA/SGD/BDG/SAB/9 baada ya mpangaji wake kushindwa kulipa deni la
shilingi 197,000.00.(Picha na Nathaniel Limu).
Sign up here with your email