Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema baada ya kubaini watumishi hewa 1,057 ambao wamesababisha hasara ya Sh2.1 bilioni, kazi iliyosalia ni kusaka waliohusika na mchezo huo mchafu na kuhakikisha fedha hizo zimerejeshwa.
Katika kufanikisha hilo, Mongella leo alitarajiwa kushiriki kikao cha mkakati ambacho kingehudhuriwa na wakuu wa wilaya zote lakini kutokana na mabadiliko ya jana hadi waapishwe wapya, makatibu tawala, wakurugenzi watendaji wa halmashauri na wakuu wa idara kwa nia ya kutoa maelekezo kwa kila mmoja.
“Kila mmoja lazima atekeleze na kutimiza wajibu katika eneo lake kuhakikisha fedha za Serikali zilizolipwa kinyume cha taratibu zinarejeshwa kugharamia miradi ya maendeleo ya wananchi,” alisema Mongella juzi.
Sign up here with your email