KAMATI YA SELEMANI MGOTO YAZITAMANI YANGA, SIMBA NA AZAM . - Rhevan Media

KAMATI YA SELEMANI MGOTO YAZITAMANI YANGA, SIMBA NA AZAM .

KAMATI ya kutafuta fedha kiasi cha sh. Mil. 18 zitakazomsaidia mkazi wa Mlandizi Selemani Mgoto kwenda nchini India kutibiwa macho, zipo katika mpango wa kuwasiliana na vikabu vya soka vya Yanga, Simba na Azam ili viweze kucheza mchezo mmoja mmoja dhidi ya vilabu vya Ruvu Shooting na JKT Ruvu za mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Eli Achahofu alisema hatua hiyo inaweza kusaidia kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha zitakazomsaidia Mhoto kwenda nvhini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya macho kutokana na upogu uliompata miaka miwli iliyopita.

Alisema kuwa mkazi huyo alitumia dawa aina ya Fansida ambayo baada ya muda ikamsababishia kupoteza kuona kama ilivyo kawaida hivyo alikwenda zahanati ya Mlandizi baadae Tumbi kabla ya kuelekea CCBRT ambako walimfanyia vipimo na kumhakikishia hayajaathirika sana hivyo akipelekwa nchini India kuna uwezekano wa kurejea katika hali yake ya kawaida.

"Tunataraji kufanya mipango ya kuwasiliana na viongozi wa vilabu hivyo waweze kutusaidia kupatikana kwa fedha hizo kwa kucheza michezo mitatu Yanga icheze na Shooting na JKT Ruvu, nazo Simba na Azam pianzicheze na timu zetu hizo za nyumbani ili tupate kiasi hicho kitachowezesha mwenzetu kuweza kusafiri kuelekea nchini India kimatibabu," alisema Achahofu.

Kwa upande wake Mhazini katika Kamati hiyo Bawazir Sematore alisema mpaka sasa Kamati hiyo imeshakusanya kiasi cha sh. Mil. 1.3 taslimi huku ahadi ikiwa ni sh. Mil. 7 amnapo bado inahitajika shilingi zaidi ya Mil. 10, ili kifikie kiwango kinachotakiwa kimsafirishe mkazi huyo.

"Juhudi bado zinaendelea imani yetu ji kwamba enfapo tutapata msaada kupitia vilabu vivyo vitano vya Yanga, Simba, Azam, Ruvu Shooting na JKT Rubu, ni imani yetu tutaweza kufikia malengo hayo, kwa sasa atayegushwa na hili awasiliane moja kwa moja na mlengwa Mgoto kupitia namba zake za mkononi 06554139390754413939 na 0787413939," alisema Sematore.

Kwa upande wake Mgoto amewaomba wa-Tanzania kokote walipo wajitokeze katika kumsaidia kuoata fedha hizo ili aweze kusafiri kwenda nchini humo kwa ajili ya kupayiwa tiba ya macho.

"Madaktari wamenihakikishia kwamba nikienda nchini India macho yangu yana asilimia 97 kurejea katika hali ya kawaida kwani vipimo vimeonesha kwamba kinachochangia gali hii ni ngozi ya nje tu macho hayajaathirika,"alimalizia Mgoto.
Previous
Next Post »