WAKATI waumini wa Dini ya
Kiislamu wakiwa ndani ya swaumu, staa wa filamu Bongo, Tiko Hassan
amefunguka kuwa na yeye yumo na ameamua kufunga kwa sababu mbili za
msingi. Akipiga stori na Ijumaa, Tiko alisema licha ya kwamba kufunga ni
nguzo muhimu ya Uislam lakini sambamba na hilo anakitumia kipindi hiki
kumuomba Mungu amjalie apate mume na afanye vizuri kwenye fani yake.
“Namshukuru Mungu kwa kunifikisha
kipindi hiki, niseme tu wazi kwamba safari hii nafunga nikinuia kabisa
kuwa Mungu anijalie nipate mume maana nimechoka kuishi maisha ya
kipweke.
“Pili, namuomba Mungu anijaalie katika
fani yangu, kurwogana kumekuwa kwingi, watu hawapendani, Mungu aniepushe
na shari,” alisema Tiko.
Sign up here with your email
