Mume wa Mwanamuziki Mariah
Carey, Nick Cannon juzikati aligoma kusaini karatasi za kuidhinisha
kumpa talaka mkewe huyo kwa madai kuwa hayuko tayari.
Kinachoonekana Nick bado anampenda mama
watoto wake huyo hivyo hayuko tayari kumuona akiolewa na tajiri James
Packer ambaye amemvalisha pete ya uchumba kwa lengo la kufunga naye
ndoa.
Nick na Mariah walitangaza kutengana
Agosti, 2014 na miezi michache baadaye walifungua mafaili ya talaka
mahakamani lakini Nick anataka kumfanyia mbaya Mariah kwa kutotaka
kumpatia talaka ili kukwamisha zoezi la ndoa.
“Nick bado ana mapenzi na Mariah na
hayuko tayari kumpoteza, hata alipovalishwa pete ya uchumba aliumia
mpaka akafikia hatua ya kulazwa hospitali, hiyo ni pete tu, ndoa je?”
alisema rafiki wa karibu wa mastaa hao alipokuwa akizungumza na mtandao
mmoja wa habari za mastaa.
Mariah na Nick walifunga ndoa ya siri mwaka 2008 kwenye Visiwa vya Nahamas na wana watoto wawili mapacha, Moroccan na Monroe.
Sign up here with your email
