SEKTA YA MAWASILIANO KUPATA MWEKEZAJI. - Rhevan Media

SEKTA YA MAWASILIANO KUPATA MWEKEZAJI.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa nia ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Oracle Afrika Bw. Cherian Varghese (katikati) akielezea nia ya Kampuni yao katika ushirikiano wa kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Dkt. Mhandisi Maria Sasabo (wa kwanza kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika walipotembelea sekta ya Mawasiliano na kueleza nia yao ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA LEO.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 (The Public Procurement Amendment Bill 2016) Leo Bungeni Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Angella Kairuki Bungeni Mjini Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa mechi hiyo yenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati nchini, kulia ni Mwenyekiti wa (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.



Previous
Next Post »