Kukakamaa kwa misuli ya uke (Vaginismus): hali hii inasababishwa na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha.
Matatizo ya shingo ya kizazi: Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi. Iwapo mwanamke ana maambukizi huisi maumivu mara shingo ya kizazi inapogusana na uume.
Matatizo katika mfuko wa uzazi: Matatizo kama fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa ngono.
Maambukizi ya uke: aina yoyote ya maambukizi ya uke kama vile maambukizi ya fangasi inaweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.
Kuumia uke: majeraha kutokana na sababu kadhaa mfano kuchanika wakati wa kujifungua au kuongeza njia katika msamba wakati wa kujifungua.
Endometriosis: Hii ni hali ambayo inasababisha tishu za mji wa mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi, na hivyo kuchochea maumivu wakati wa kukutana kimwili.
Maambukizi kwenye funga nyonga(PID): Viungo kwenye nyonga vinaweza kupata maambukizi hivyo kusababisha maumivu wakati wa ngono.
Matatizo ya ovari: Matatizo haya ni pamoja na uvimbe kwenye mfuko wa mayai (ovarian cyst)
Wanakuwa waliokoma siku(Menapause): Wakati wanapokuwa wamekoma siku zao maumbile yao yanasinyaa na kuwa kavu, hivyo kuchochea maumivu wakati wa tendo la ndoa
Magonjwa ya zinaa: magonjwa ya zinaa kama malengelenge (herpes), masundosundo n.k, yanaweza kusababisha maumivu wakati wa ngono.
Sign up here with your email