………………………………………………………………………………………………..
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametoa
miezi mitatu kwa Kampuni ya SINO HYDRO COMPANY LIMITED inayojenga
Barabara ya Dodoma-Mayamaya kwa kiwango cha Lami kuhakikisha barabara
hiyo inakamilika.
Akizungumza
mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo yeye urefu
wa kilomita 43.6 Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi kuikabidhi barabara
kwa Serikali ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
“Hakikisheni
barabara hii ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Great North Road
inakamilika ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kukamilisha barabara
hiyo eneo la Tanzania kwa kiwango cha lami, amesema Waziri Prof.
Mbarawa.
Barabara
ya Dodoma-Mayamaya ni sehemu ya Barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati yenye
urefu wa Kilomita 247.8 ambayo ujenzi wake umegawanywa sehemu tatu
ambazo ni Dodoma-Mayamaya KM 43.6, Mayamaya-Mela-Bonga KM 188.15.
‘Kukamilika
kwa barabara hii ambayo ni sehemu ya Barabara Kuu ya Great North Road
inayoanzia Capetown Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri kutachochea
fursa za kibiashara na kiuchumi katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi za Kaskazini mwa Afrika’, amesisitiza
Prof. Mbarawa
Mpaka
sasa takribani shilingi bilioni 43 zimeshalipwa kwa mkadarasi SINO
HYDRO COMPANY LIMITED kukamilisha kilimilisha KM 8 zilizobaki katika
sehemu ya Dodoma-Mayamaya, barabara ambayo ambayo imejengwa kwa viwango
vinavyokubalika.
Barabara
ya Great North Road inayopita mikoa ya Iringa, Dodoma na Arusha
inaanzia Capetown Afrika Kusini hadi Cairo Misri mbapo kukamilika kwake
kutaliunganisha Bara la Afrika kwa Barabara ya Lami.
Sign up here with your email
