Mkali
wa Hip Hop Kalla Jeremiaha ameongea na Enews na kueleza sababu
zinazopelekea yeye kuonekana kama amepotea kwenye muziki na kusema sio
kweli kwamba kapotea bali ni kwa sababu za kujiweka mbali na kiki zisizo
na msingi.
Hata
hivyo Kalla ameelezea jina la mtoto wake ambaye ni takribani miezi 3
tangu azaliwe huku akitoa sababu zilizopelekea yeye kumuita mtoto wake
“ALAMA” na kusema ni neno la kiswahili na kwamba anadumisha lugha yake
kwani angemuita kwa lugha ya kingereza jina lake lingekuwa 'Mark'
Amesema
jina hilo halijaleta matatizo yoyote kwa mtoto wake tofauti na watu
wanavyosema usipomuita mtoto jina la asili anakuwa anasumbua kwa kulia
au kuumwaumwa ila kwa mtoto wa Kalla imekuwa tofauti kabisaa.
Sign up here with your email
