Msanii
Malaika amezidi kuwaweka watu mbali mbali kwenye kigugumizi juu ya
tetesi za yeye ni mshirika wa dini ya kishetani, free mason.
Malaika
ambaye wachunguzi wa mambo wamesema anapenda kutumia namba inayohushwa
na imani hiyo ya kishetani ya 666, ambayo hata namba yake ya simu
inaishia 666, amesema hatolizungumzia suala hilo alipokuwa akiongea na
Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema muda muafaka utakapofika
ataweka wazi kila kitu.
“Sitopenda
kuizungumzia ila niseme tu kwamba ni namba ambayo naipenda, nimepata
simu nyingi sana, interviews lakini siku nitakayoamua kuongelea
nitaongea kuhusu hivyo, lakini kwa sasa hivi siko tayari”, alisema
Malaika.
Pia
Malaika amesema hata jina lake la Malaika ambalo watu wanamtuhumu
haendani nalo kutokana na mambo hayo, amesema hajali kuhusu hilo kwani
hilo ni jina tu kama jina lingine.
Kwenye akaunti yake ya instagram, Malaika ameandika wasifu wenye kushtua watu, ambao amehusisha na Illuminati ndani yake.
Sign up here with your email
