Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa
mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko
hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi.
Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
- Arusha – Mrisho Mashaka Gambo
- Arumeru – Alexander Pastory Mnyeti
- Ngorongoro – Rashid Mfaume Taka
- Longido – Daniel Geofrey Chongolo
- Monduli – Idd Hassan Kimanta
- Karatu – Therezia Jonathan Mahongo
- Kinondoni – Ally Hapi
- Ilala – Sophia Mjema
- Temeke – Felix Jackson Lyaviva
- Kigamboni – Hashim Shaibu Mgandilwa
- Ubungo – Hamphrey Polepole
- Chamwino – Vumilia Justine Nyamoga
- Dodoma – Christina Solomon Mndeme
- Chemba – Simon Ezekiel Odunga
- Kondoa – Sezeria Veneranda Makutta
- Bahi – Elizabeth Simon
- Mpwapwa – Jabir Mussa Shekimweli
- Kongwa – John Ernest Palingo
- Bukombe – Josephat Maganga
- Mbogwe – Matha John Mkupasi
- Nyang’wale – Hamim Buzohera Gwiyama
- Geita – Herman C. Kipufi
- Chato – Shaaban Athuman Ntarambe
- Mufindi – Jamhuri David William
- Kilolo – Asia Juma Abdallah
- Iringa – Richard Kasesela
- Biharamulo – Saada Abraham Mallunde
- Karagwe – Geofrey Muheluka Ayoub
- Muleba – Richard Henry Ruyango
- Kyerwa – Shaban Ilangu Lissu
- Bukoba – Deodatus Lucas Kinawilo
- Ngara – Col. Michael M. Mtenjele
- Missenyi – Col Denis F. Mwila
- Mlele – Rachiel Stephano Kasanda
- Mpanda – Lilian Charles Matinga
- Tanganyika – Saleh Mbwana Mhando
- Kigoma – Samsoni Renard Anga
- Kasulu – Martin Elia Mkisi
- Kakonko – Hosea Malonda Ndagala
- Uvinza – Mwanamvua Hoza Mlindoko
- Buhigwe – Elisha Marco Gagisti
- Kibondo – Luis Peter Bura
- Siha – Onesmo Buswelu
- Moshi – Kippi Warioba
- Mwanga – Aaron Yeseya Mmbago
- Rombo – Fatma Hassan Toufiq
- Hai – Gelasius Byakanwa
- Same – Rosemary Senyamule Sitaki
- Nachingwea – Rukia Akhibu Muwango
- Ruangwa – Joseph Joseph Mkirikiti
- Liwale – Sarah Vicent Chiwamba
- Lindi – Shaibu Issa Ndemanga
- Kilwa – Christopher Emil Ngubiagai
- Babati – Raymond H. Mushi
- Mbulu – Chelestion Simba M. Mofungu
- Hanang’ – Sara Msafiri Ally
- Kiteto – Tumaini Benson Magessa
- Simanjiro – Zephania Adriano Chaula
- Rorya – Simon K. Chacha
- Serengeti – Emile Yotham Ntakamulenga
- Bunda – Lydia Simeon Bupilipili
- Butiama – Anarose Nyamubi
- Tarime – Glodious Benard Luoga
- Musoma – Vicent Anney Naano
- Chunya – Rehema Manase Madusa
- Kyela – Claudia Undalusyege Kitta
- Mbeya – William Ntinika Paul
- Rungwe – Chalya Julius Nyangidu
- Mbarali – Reuben Ndiza Mfune
- Gairo – Siriel Shaid Mchembe
- Kilombero – James Mugendi Ihunyo
- Mvomero – Mohamed Mussa Utali
- Morogoro – Regina Reginald Chonjo
- Ulanga – Kassema Jacob Joseph
- Kilosa – Adam Idd Mgoyi
- Malinyi – Majula Mateko Kasika
- Newala – Aziza Ally Mangosongo
- Nanyumbu – Joakim Wangabo
- Mtwara – Khatibu Malimi Kazungu
- Masasi – Seleman Mzee Seleman
- Tandahimba – Sebastian M. Walyuba
- Ilemela – Leonald Moses Massale
- Kwimba – Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
- Sengerema – Emmanuel Enock Kipole
- Nyamagana – Mary Tesha Onesmo
- Magu – Hadija Rashid Nyembo
- Ukerewe – Estomihn Fransis Chang’ah
- Misungwi – Juma Sweda
- Njombe – Ruth Blasio Msafiri
- Ludewa – Andrea Axwesso Tsere
- Wanging’ombe – Ally Mohamed Kassige
- Makete – Veronica Kessy
- Bagamoyo – Alhaji Majid Hemed Mwanga
- Mkuranga – Filberto H. Sanga
- Rufiji – Juma Abdallah Njwayo
- Mafia – Shaibu Ahamed Nunduma
- Kibaha – Asumpter Nsunju Mshama
- Kisarawe – Happyness Seneda William
- Kibiti – Gulamu Hussein Shaban Kifu
- Sumbawanga – Khalfan Boniface Haule
- Nkasi – Said Mohamed Mtanda
- Kalambo – Julieth Nkembanyi Binyura
- Namtumbo – Luckness Adrian Amlima
- Mbinga – Cosmas Nyano Nshenye
- Nyasa – Isabera Octava Chilumba
- Tunduru – Juma Homela
- Songea – Polet Kamando Mgema
- Kishapu – Nyambonga Daudi Taraba
- Kahama – Fadhili Nkulu
- Shinyanga – Josephine Rabby Matiro
- Busega – Tano Seif Mwera
- Maswa – Sefu Abdallah Shekalaghe
- Bariadi – Festo Sheimu Kiswaga
- Meatu – Joseph Elieza Chilongani
- Itilima – Benson Salehe Kilangi
- Mkalama – Jackson Jonas Masako
- Manyoni – Mwembe Idephonce Geofrey
- Singida – Elias Choro John Tarimo
- Ikungi – Fikiri Avias Said
- Iramba – Emmanuel Jumanne Luhahula
- Songwe – Samwel Jeremiah
- Ileje – Joseph Modest Mkude
- Mbozi – Ally Masoud Maswanya
- Momba – Juma Said Irando
- Nzega – Geofrey William Ngudula
- Kaliua – Busalama Abel Yeji
- Igunga – Mwaipopo John Gabriel
- Sikonge – Peres Boniphace Magiri
- Tabora – Queen Mwashinga Mlozi
- Urambo – Angelina John Kwingwa
- Uyui – Gabriel Simon Mnyele
- Tanga – Thobias Mwilapwa
- Muheza – Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
- Mkinga – Yona Lucas Maki
- Pangani – Zainab Abdallah Issa
- Handeni – Godwin Crydon Gondwe
- Korogwe – Robert Gabriel
- Kilindi – Sauda Salum Mtondoo
- Lushoto – Januari Sigareti Lugangika
BWANA HARUSI AFARIKI
KWA AJALI BAADA YA SEND OFF
Gerson Ngassalah enzi za uhai wake akiwa na Gerson Ngassalah enzi za
uhai wake akiwa na mchumba wake Felister Ngowi.
Mbeya. Maisha ya mtu ni siri ya Muumba wake na wakati ukifika hana budi
kuyakatisha.
Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya ndoto za Gerson Ngassalah (27)
mkazi wa Kalobe jijini Mbeya za kufurahia maisha baada ya kuachana na
ukapera kuzimwa ghafla alfajiri ya Jumatano iliyopita katika ajali
iliyosababisha kupoteza uhai wake papo hapo, siku moja kabla ya harusi
yake.
Gerson alipata ajali hiyo katika maeneo ya Makambako akiwa njiani
kurejea jijini Mbeya akitokea Dar es Salaam alikokwenda kwenye send-off
ya mchumba wake, Felister Ngowi iliyofanyika Jumatatu katika maeneo ya
Sinza.
Harusi ya wawili hao ilitarajiwa kufanyika Alhamisi jijini Mbeya lakini
Gerson hakuifikia akimuacha mchumba wake akiwa mjamzito.
Badala ya siku hiyo kuwa ya furaha, ikawa ndiyo ya mazishi ya kijana
huyo.
Akizungumza nyumbani kwa wazazi wao, Emmanuel Ngassalah ambaye ni kaka
mkubwa wa marehemu alisema Jumatatu ya Juni 20, marehemu akiambatana na
ndugu zao wengine walihudhuria sherehe ya kumuaga mchumba wake na baada
ya shughuli hiyo walitawanyika kurudi nyumbani kwa ajili ya kujiandaa na
safari ya kurejea Mbeya.
“Kesho yake (Jumanne) mdogo wangu pamoja na ndugu wengine walianza
safari saa moja jioni kuja Mbeya kuwahi harusi na mchumba wake
alishakatiwa tiketi ya ndege na mchumba wake na alisafiri Jumatano
asubuhi akiwa na mama yake mdogo,” alisema Emmanuel.
Alisema katika msafara wa bwana harusi walikuwa na magari mawili, Gerson
na ndugu zake watano na jingine ambalo lilibeba watu sita lililokuwa
mbele.
Emmanuel alisema gari la mbele liliwaacha umbali wa kilomita 100 hivi na
walipofika njia panda ya Ilembula (Njombe) alfajiri ya saa kumi na
moja, mmoja wao alimpigia simu na dada yetu Aines, akiwajulisha kwamba
wamepata ajali, gari lao limepinduka eneo la Chimba dawa – Makambako,
hivyo warudi haraka.
Alisema walipofika pale walimkuta Gerson akiwa amepoteza fahamu,
mwingine akiwa amevunjika mguu lakini watatu wakiwa salama, hivyo
kumpeleka Hospitali ya Ilembula lakini walipofika madaktari waliwaambia
ndugu yao amepoteza maisha.
“Basi hapo kukawa hakuna namna nyingine, ukafanyika utaratibu wa kubeba
mwili wa marehemu hadi Mbeya.
Alisema asubuhi hiyo saa mbili, mchumba wa marehemu naye alifika akiwa
na mama yake mdogo na walikwenda moja kwa moja hotelini walikopanga
kufikia na Gerson.
Mchumba azimia
Emmanuel alisema baada ya mchumba wake kupata taarifa kuwa mumewe
mtarajiwa hayupo tena duniani, alilia kwa uchungu na wakati wa kuweka
mashada ya maua makaburini, aliishiwa nguvu na kuanguka na walipelekwa
Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambako ilibainika kuwa ameishiwa maji. Baada
ya matibabu, aliruhusiwa kutoka Ijumaa iliyopita.
“Kwa sasa hutaweza kumuona wala kuzungumza naye, huyu binti hayupo
vizuri kabisa. Tunajitahidi kumfanyia ushauri ili aweze kurudi katika
hali yake japo itamchukua muda kidogo kuwa sawa,” alisema Emmanuel.
Baba Mdogo wa Felister, Jonathan Ngowi alisema wakiwa safarini kwenda
Mbeya kwa ajili ya harusi na mtoto wao walipokea simu kutoka kwa binamu
yake kwamba mambo yameharibika kwani mkwe wao ameoteza maisha katika
ajali.
“Mipango ya Mola ikageuza furaha kuwa msiba mzito kwetu sote. Hatuna
namna nyingine tunamuachia Mola mwenyewe,” alisema Ngowi na kuongeza:
“Kwenye gari tulikuwa watano, nilipopokea simu ile kutoka kwa binamu
yangu, akawa ananiuliza vitu ambavyo sikumuelewa kabisa na ghafla
akakata simu, lakini mimi nikampigia tena bado akawa anababaika kusema,
mwisho nikamwambia niambie kuna tatizo gani?
“Baadaye akaniambia, bwana mpo safarini lakini huko mnakokwenda siyo
salama kabisa, mkwe wenu amepata ajali na amefariki. Hapo nikakaa zaidi
ya dakika 10 bila kusema chochote, baadaye mke wangu akaniuliza
‘kulikoni mbona upo kimya tangu umalize kuongea na simu?’”
Alisema alichelewa kidogo kumweleza mke wake kwa kuwa nyuma ya gari hilo
walikuwa wamekaa wazazi wa Felister, lakini hakuwa na namna yoyote ile
ikambidi amnong’oneze tu mkewe, ndipo wakaambizana kukaa kimya bila ya
kuwaambia hadi watakapofika Mbeya.
“Lakini ghafla taarifa zikaenea kwenye mitandao ya kijamii (WhatsApp),
kuna mtu alipopata taarifa hizo akaamua kuzirusha, ndipo akazipata ndugu
yao mwingine ambaye alimpigia baba wa Felister kumuuliza juu ya taarifa
hizo.”
Alisema baada ya kuona hivyo, ikabidi amuweke wazi kwamba ni kweli tukio
hilo lipo na ameshapewa taarifa na binamu yake aliyekuwa mshenga,
lakini akawaeleza kwamba hawana namna nyingine ni lazima wafike Mbeya
kwenye msiba badala ya harusi.
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Sign up here with your email