Na Musa Mateja, RISASI MCHANGANYIKO
DAR ES SALAAM: Katika hali ya
kushangaza, staa wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’
amenaswa akimdhalilisha staa mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kwa
kumshika sehemu zake nyeti.
Tukio hilo la aina yake lilijiri
wikiendi iliyopita katika Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar
kulipokuwa na shoo ya kuadhimisha miaka kumi ya staa wa Muziki wa Dansi,
Christian Bella ‘Obama’.
Paparazi wetu aliyekuwa akifanya ziara
ya kushtukiza mara kwa mara back stage, kuna wakati alifanikiwa kumkuta
Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo
akionekana kumpa ushirikiano.
“Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama
wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani?
Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa
mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.
Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana
na tukio hilo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Baraka, Linah alidai
haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.
“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.
Kwa upande wake Baraka ambaye
inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia
chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.
Linah na Baraka waliwahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake hadi
waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo.
Sign up here with your email
