MOROGORO: Mfanyabiashara maarufu
nchini, Abubakari Msofe maarufu kama Papaa Msofe, wiki iliyopita
aliwamwagia warembo minoti wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa
Mkoa wa Morogoro, lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashera.
Mfanyabiashara huyo aliyekuwa mgeni
rasmi kwenye shughuli hiyo, alitoa kiasi kikubwa cha fedha pia kwa
mshindi wa kwanza ambaye pia alikabidhiwa shilingi laki tatu kwa kuibuka
kidedea.
Papaa Msofe ni mfanyabiashara ambaye
alikaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kudaiwa kuhusika na
mauaji ya Onesphory Kituli kabla ya kuachiwa mwishoni mwa mwaka jana
baada ya kufutiwa shtaka hilo na kubadilishiwa lingine ambalo ni la
kughushi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Sign up here with your email
