Aidha, Lukuvi amezitaka benki kuacha kuuza nyumba za wateja wanaposhindwa kulipa deni hata kama kiasi kilichobakia ni kidogo.
Aliwaonya kuacha kutamani nyumba za wateja wao akisema kuwa kuna baadhi ya benki hujifanya kuuza nyumba za wateja wao kwa bei ndogo wakati zimeuza kwa gharama kubwa.
Lukuvi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wadau wa sekta ya uendelezaji milki ambapo alisema wamiliki wa nyumba wamekuwa wakiwanyanyasa wapangaji kwa kuwaongezea kodi kila kukicha licha ya kwamba baadhi ya nyumba haziendani na thamani ya fedha zinazotolewa.
“Wapangaji wanapata shida, wananyanyaswa na wenye nyumba kila kukicha wanapangishiwa kodi na nyumba sasa lazima tufanye utaratibu wa kudhibiti suala hilo na ikibidi bei elekezi,” alisema.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, serikali itaanzisha chombo maalumu kwa ajili ya kudhibiti upandishwa wa kodi kwa wapangaji.
“Kuna wengine wakikuona umenunua runinga ya kisasa anakupandishia kodi, sasa hatuwezi kwenda kwa namna hii lazima kiwepo chombo cha kusimamia haki za wapangaji," alisema Lukuvi "Tutatunga sheria ambayo itawasimamia.”
Alisema mpangaji anatakiwa kulipa kodi ambayo inaendana na nyumba anayotaka kupanga.
Aidha, alizitaka benki kuacha mchezo wa kuuza nyumba za wateja wao kienyeji na badala yake wawe wanawasaidia ili kuwawezesha na wenyewe kupata faida.
Aidha, alizitaka benki kuacha mchezo wa kuuza nyumba za wateja wao kienyeji na badala yake wawe wanawasaidia ili kuwawezesha na wenyewe kupata faida.
“Utakuta mteja anadaiwa Sh. milioni 5 nyumba inauzwa kwa gharama ndogo na si kweli kwamba imeuzwa kwa bei ndogo bali huo unakuwa ni mchezo unafanywa na watumishi wa benki husika,” alisema.
Aidha, Lukuvi aliligeukia Shirika la Nyuamba (NHC) na wauzaji wengine wa nyumba kuwa wamekuwa wakiziuza kwa gharama kubwa ambazo mtanzania mwenye kipato cha chini hawezi kununua.
“Unakuta nyumba ndogo ya vyumba viwili inauzwa Sh. milioni 50, tena inatangazwa kwamba ni nyumba ya bei nafuu… nikiwa na kiwanja ukanipa Sh. milioni 50 nitajenga nyumba yangu kubwa tofauti na hivyo vyumba viwili,” alisema.
Lukuvu alisema taasisi za umma pamoja na nyingine ambazo zinauza nyumba kwa wananchi zinatakiwa kuangalia bei halisi na siyo kuwaibia wananchi.
Alisema nyumba nyingi ambazo zinauzwa zinawalenga wale wenye kipato kikubwa huku wananchi wa kawaida wakishindwa kuzinunua.
Lukuvi aliwataka wauze nyumba kwa gharama nafuu ili wananchi waweze kuzinunua.
“Kuna mwekezaji mmoja anatokea Babati ataeleza jinsi alivyoweza kumudu kujenga nyumba na kuziuza kwa Sh. milioni 15," alisema.
“Kuna mwekezaji mmoja anatokea Babati ataeleza jinsi alivyoweza kumudu kujenga nyumba na kuziuza kwa Sh. milioni 15," alisema.
"Kama huyu kaweza kujenga kwa bei hiyo na vifaa vya ujenzi vinatokea Dar es Salaam na wale wanaojenga kwa ujenzi wa Dar es Salaam inakuwa na gharama kubwa ya Sh. milioni 50.
“Ukienda mtaani ukiangalia vifaa pamoja na bati zilizotumika bei halisi haihitaji kwenda shule gharama bado ni kubwa.”
Sign up here with your email