Makonda alieleza mkakati huo wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabishara Tanzania (JWT) katika mkutano wao wa mwaka uliojumuisha wafanyabiashara kutoka mikoa yote nchini.
Makonda ambaye ni mmoja wa wakuu wa mikoa walioapishwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo Machi 15, alisema lengo la kufunga taa ni kuwezesha biashara hadi usiku na kutekeleza kwa vitendo dhana ya Jiji hilo kuwa la kibiashara.
Matukio ya uvamizi wa wafanyabiashara katika sehemu zao usiku kutoka ama kwa majambazi au vikundi vya uporaji kama Panya Road, yamekuwa yakifanya maduka mengi kufungwa mapema jijini.
“Juzi usiku nilifanya ziara ya kukagua taa za barabarani, jambo la kushangaza nilikuta sehemu kubwa ya mji ikiwa ni giza," alisema.
"Hivyo tumeshaanza kufunga taa katika maeneo yote ili kulipendezesha Jiji lakini pia wafanyabishara wafanyebiashara hadi usiku.”
Alisema wafanyabishata walimueleza kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya biashara hadi usiku kwa sababu ya kukosa mwanga wa kutosha na kutokuwepo na usalama wa mali zao.
“Ni jambo la aibu wafanyabishara wa Kariakoo wanashindwa kufanya biashara zao hadi usiku… wanalazimika kufunga jioni wakati kuna watu wanatoka kazini usiku na wanataka kununua bidhaa.”
Makonda alisema changamoto zote ameanza kuvifanyia kazi na kwamba atatumia askari polisi zaidi ya 300 wa jiji kulinda usalama wa raia na mali
Sign up here with your email