Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amesema kuwa atahakikisha heshima
ya tasnia ya habari inarudi baada ya kupitishwa kwa mswada wa sheria ya huduma za
vyombo vya Habari.
Waziri Nape ameyasema hayo alipokuwa katika katika ziara mkoani Mara na Shinyanga
na kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara hiyo na kupokea taarifa ya mkoa
na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mikoa hiyo.
“Ule mswada utatoa tafsiri ya mwandishi wa habari,maana mwandishi wa habari
lazma awe na sifa.Siku hizi anaweza kuwa mtu anauza ndizi alafu akajifunza kupiga
picha akajiita na yeye mwandishi wa Habari.Ukifanya ivyo tasnia hii inakosa
heshima,kwaiyo sheria ile itatafsiri nani mwandishi wa habari”Alisema Nape.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau waliopo chiniya wizara yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan(wa kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura Kajala.
Aidha Waziri Nape alisema kuwa kwa kufanya hivi sheria hii itatibu tatizo la kulipwa
vibaya na wamiliki wa vyombo vya habari maana mwandishi huyu atakuwa na
elimu,maana kama hana elimu mmiliki ataajili mtu anaejua kusema wa kijuweni alafu
ndo anamuajiri anakuwa mtangazaji wa radio yake kisa tu anajua kusema.
Pamoja na hayo waziri uyo mwenye dhamana ya wizara nyeti ya habari alisema kuwa
sheria hiyo pia itazungumzia maslahi ya mwandishi wa habari,itawabana wamiliki na
mswada huu ukipita utarudisha heshima ya tasnia hii ya habari katika nchi yetu.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Josephine Matiro akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye baada ya kuwasili mkoani hapo ili kujua changamoto mbalimbali za watumishi walio chini ya wizara yake na kuongea na wadau wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Akizungumzia upande wa radio kujenga nchi waziri nape amewaasa waandishi wa
habari na watangazaji wa radio kujenga amani ya nchi yetu kwa kuwaunganisha
watanzania kupitia radio zao na si kuwatenganisha akitolea mfano wa yaliyotokea
nchini Rwanda kwamba radio zilitumika kuhamasisha mauaji.
Mheshimiwa Nape pia amehaidi kuimarisha vitengo vya mawasiliano serikalini ikiwa ni
pamoja na kuwapa maafisa hao vitendea kazi, pia ameliomba jeshi la polisi kutoa
ushirikiano katika kutoa taarifa na amehaidi kuzungumza na jeshi hilo ili waandishi
hawa waweze kupata taarifa kirahisi.
Waziri uyo yupo katika ziara ya mikoa ya Kagera,Mara,Shinyanga,Tabora na Singida
ikiwa na lengo kuu la kuileta Wizara ya habari,utamaduni,Sanaa na Michezo mikoani
na wilayani karibu na wadau.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) mkoani Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe(mwenye kofia ya njano) kuhusu maendelezo ya uwanja wa kambarage ambao unamilikiwa na chama hicho mkoani hapo.Mhe.Nape amewaasa viongozi wa mkoa huo kutafta wadhamini ili kuuboresha uwanja huo.
Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan akizungumza na wadau mbali mbali wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na watumishi wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye mkoani humo. serikali wa mkoa wa Mara leo hii wakati wa Ziara ya Waziri wa
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo mwandamizi wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bw.John Igomego jinsi mitambo yakurushia matangazo ya shirika hilo inavyofanya kazi mkoa wa Mara.
Sign up here with your email