Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza kukamatwa kwa afisa ardhi wa halmashauri ya musoma kwa kosa la kutoa hati ya kiwanja katika eneo la mnada wa serikali.
Nimefika eneo la mnada wa upili wa Kirumi-Butiama(mnada wa ng'ombe).Nimesikitishwa kuona eneo la serikali lililotengwa kwaajili ya mnada na lina hati,sehemu ya eneo limeuzwa kwa mtu mwingine binafsi na kukwamisha shughuli za mnada.Ni kitendo kisichokubalika na hakivumiliki,nimeagiza afisa ardhi aliyehusika na mchezo huu mchafu akamatwe na hatua za kisheria zifuate. Migogoro ya namna hii wakati wake umeshafika mwisho,watumishi wa serikali fanyeni kazi ya kuongoza na kuonesha njia,tutumie ofisi za umma kusaidia kutatua kero na sio kusababisha kero.
Sign up here with your email