Mchezaji nyota wa klabu ya Newcastle United ya Uingereza amepigwa faini na hakimu na kisha akatakiwa heri katika Ligi ya Premia.
Mshambuliaji Papiss Cisse, kutoka Senegal, aliadhibiwa baada ya kupatikana na kosa la trafiki.
Alikuwa amepewa leseni ya kuendesha magari mwaka mmoja nchini Uingereza lakini amekuwa akitumia leseni hiyo kwa miaka mitatu.
Cisse, 30, anayeishi Darras Hall, Ponteland, alipewa alama nne na akapigwa faini £547 na mahakimu Newcastle.
Klabu yake inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja katika Ligi Kuu ya England na baada ya kumsomea hukumu, mwenyekiti wa jopo la mahakimu Carolyn Hyslop kisha alimwambia: "Kila la kheri kesho."
Newcastle United watakutana na Swansea City uwanjani St James' Park Jumamosi kwenye mechi ambayo wanahitajika kushinda kujiongezea matumaini ya kunusurika.
Sign up here with your email