UPANDISHWAJI WA MADARAJA WALIMU WAZUA TAHARUKI. - Rhevan Media

UPANDISHWAJI WA MADARAJA WALIMU WAZUA TAHARUKI.















Na Woinde Shizza,Arusha

Baadhi ya walimu wa jiji la Arusha wamelalamikia utaratibu uliotumika wa upandishwaji wa madaraja na kusema kuwa utaratibu huo ni ujawatendea haki walimu waliofanya kazi kwa kipindi kirefu pamoja na wale ambao wamestaafu
Walimu hao walisema kuwa utaratibu uliotumika wa kuwachanganya walimu waliofanya kazi kwa kipindi cha mda mrefu zaidi ya miaka 20 pamoja na walimu wageni ambao wengine hawana mda mrefu kazini kwani wamefanya kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu ni mbovu na unawakatisha tama ya kufanya kazi kwa umakini.

Mmoja wa walimu hao aliyejitambulisha kwa jina la Mark Mbwabwo alisema kuwa mfumo huo wa upandishwaji wa madaraja haukuwatendea haki kabisa walimu ambao wamefanya kazi kwa kipindi cha mda mrefu kwani katika swala la ulipwaji mshahara mnakuta mwalimu aliefanya kazi kwa kipindi cha miaka 20 analipwa sawa na mwalimu ambaye amefanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja au mitatu.

Gazeti hili lilitembelea ofisi ya chama cha walimu (CWT) mkoa wa Arusha ili kujua kama wamepata malamiko hayo ambayo yalitolewa na baadhi ya walimu ambao wamepandishwa madaraja na kukutana na katibu wa chama cha walimu Halmashauri ya jiji la Arusha Magreth Hovokela ambapo alitolea ufafanuzi tuhuma hizo na hatua ambazo wao kama chama cha walimu wamezifikia.

Katika ufafanuzi wake alisema kuwa swala la upandishwaji wa madaraja kwa walimu waliogota ni la mda mrefu kwani wao kama CWT walipeleka pendekezo hilo tangu December 17 mwa ka 2014 na serekali ikakubali kupandisha walimu waliogota kwa kipind cha muda mrefu , serekali ilisema kuwa walimu hao wanaopandishwa madaraja wapandishwe kutokana na muundo wa zamani ambapo ilipitishwa walimu wapandishwe kuanzia mapema July 1 ,2015 lakini swala hilo halikutekelezeka.

Aidha aliongeza kuwa swala hilo alikutekelezwa kwa kipindi hicho na lilianza kutekelezwa rasmi January 1 hadi machi mwaka huu na kila halmashauri imeshaanza kutekeleza swala hilo kutokana na ilivyojipanga pamoja na bajeti yake na katika barua ambazo walimu wamepewa za kupandishwa madaraja zinaainisha kuwa walimu hao wamepanda madaraja kuanzia January 1 mwaka huu badala ya July 7,2015 kama vile waraka unavyoelekeza.



Previous
Next Post »