Aidha, wamebainika kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 92.
Dk. Kebwe pia amewasimamisha kazi maofisa wawili wa halmashauri hiyo kwa kushindwa kufuatilia mapato kwa kipindi cha miaka sita mfululizo.
Alitoa maagizo hayo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mgodi wa mawe ya kutengenezea marumaru, unaoendeshwa na kampuni ya Zhan Fa Construction Material Group, Kijiji cha Maseyu, Tarafa ya Mikese, wilayani Morogoro.
Alisema amelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kubaini kampuni hiyo ikiendesha mgodi huo kinyume na sheria baada ya kufungiwa na serikali tangu mwaka 2010, lakini bado waliendelea na uzalishaji, na kuagiza kukamatwa kwa wafanyakazi watatu wa mgodi huo.
Aliagiza kukamatwa kwa Shiqing Liang ,Wang Jun na Hilary Paul, na kuwasimamisha kazi maofisa wawili wa halmashauri hiyo akiwamo Ofisa Mipango, Joel Mkesela na Ofisa Biashara, Denis Lyepa, kwa kushindwa kufuatilia mapato ya halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka sita mfululizo.
Wakati akitembelea maeneo mbalimbali ya mgodi huo, alibaini kuendelea kwa shughuli nyingine za usafishaji wa madini ya dhahabu kinyume na sheria, na kukuta mifuko ya sandarusi maarufu kama viroba ikiwa na mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya dhahabu, tayari kusafirishwa.
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro akiwamo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Kibena Kingo na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba, walisema mgodi huo ulikuwa ukikwepa kodi na kuwaathiri katika mapato ya halmashauri.
Sign up here with your email