Siku cha chache tu baada wanawake wawili vikongwe kuuawa kinyama kwa imani za ushirikina katika kijiji cha Kenyamusana wilayani Rorya,serikali mkoani Mara imeufuta uongozi wote wa serikali ya kijiji hicho ikiwa ni pamoja kumsimamisha kazi Afisa Mtendaji wa kata ya Baraki kwa madai ya kushindwa kuzuia mauaji hayo ya kikatili.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw Magesa Mulongo,amechukua uamuzi huo baada ya kufika katika kijiji hicho na kusema kuwa mipango ya mauaji ya wanawake hao vikongwe imefanyika mchana kweupe lakini viongizi hao kijiji na kata walishindwa kuchukua hatua za kuzuia mauaji hayo kabla ya kutokea.
kiongozi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Mara,ameliagiza jeshi kufanya uchunguzi wa haraka na kuhakikisha watu wote walihusika kufanya mauaji hayo ya kinyama wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Naye Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Tarime na Rorya Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Andrew Satta,amesema tayari watu 14 wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku akiwataka watu wote waliohusika kufanya unyama huo kujisalimisha wenyewe.
Wiki iliyopita kundi la watu katika kijiji hicho waliwaua kwa kuwakata mapanga kisha kuwachoma moto wanawake wawili vikongwe kwa tuhumu za kujihusisha na ushirikina,tukio ambalo limesababisha hofu kubwa kwa wanawake wengi wenye umrimkubwa katika kijiji hicho.
Sign up here with your email